Sunday, November 28, 2010

REAL MADRID FC KUPAMBANA NA BARCELONA FC -KESHO

Lile pambano linalosubiriwa kwa hamu la miamba ya soka nchini Hispania,Real Madrid na Barcelona, limewadia. Zikiwa zimebakia saa chache wachezaji wa pande zote mbili wanaashiria kutoogopa timu pinzani au mpambano huo kwa ujumla.
Real Madrid chini ya kocha Jose Mourinho, inaingia kwenye pambano hilo ikiwa haijapoteza mchezo kwa kushinda mechi kumi na sare mbili.Kwa upande wa Barcelona wao wana rekodi ya kushinda mechi kumi sare moja na kupoteza mchezo mmoja.
Kukiwa hakuna majeruhi kwa pande zote mbili, mpambano huo unatarajiwa kuwa mkali kwani kumbukumbu zinaonyesha, toka walipokutana kwa mara ya kwanza mwaka 1902, Madrid imeshinda mara 85 na Barcelona 81 huku kukiwa na sare 42.
Mchezaji nyota wa Real Madrid, Christiano Ronaldo amesema wao wanakwenda Camp Nou kwa nia ya kutafuta ushindi na si vinginevyo wakati Lionel Messi,mshambuliaji hatari wa Barcelona, raia wa Argentina, alikaririwa akisema hivi karibuni kwamba Barcelona bado ni timu bora kuliko wapinzani wao, ingawa anakubali kuwa bidii na moto wa Madrid mwaka huu ni tofauti na misimu miwili iliyopita.
Mourinho anatarajia kupunguza “uteja” wa Madrid kwa Barcelona chini ya Guardiola, wakati Mourinho akitamba kuujua mpambano huo hata akiwa usingizini.Madrid hawajaifunga Barcelona nyumbani toka desemba ya 2007 na Mourinho ameshaifunga Barcelona akiwa kocha wa Chelsea na Inter Milan.Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kocha Jose Mourinho kuiongoza Real Madrid katika mpambano na Barcelona.
Ushindi katika El Classico unachukuliwa kuwa ni ishara ya ushindi wa ligi kwani katika misimu sita iliyopita, mshindi wa mpambano huu ndiye aliyechukua kombe mwisho wa msimu.Jumla ya mashabiki 98,000 wanatarajiwa kushuhudia mpambano huo ndani ya Uwanja wa nyumbani wa Barcelona,Nou Camp,huku mamilioni ya mashabiki wa soka ulimwenguni wanatarajiwa kuufuatilia mpambano huo kupitia luninga na mtandaoni.

Nyota wa pande zote mbili wamekuwa na ari ya kutaka kuonyesha vipaji na uwezo wao wakati Ronaldo na Messi wakimimina mvua za magoli katika mechi za karibuni.Huu unaaminika kuwa pia mpambano baina ya Ronaldo na Messi katika kuonyesha nani ni bora zaidi miongoni mwao.
Zote hizi ni dondoo tu, mpira huchezwa kwa dakika tisini.Tusubiri matokeo.
Written by E.Manambi with additional notes by Jeff Msangi


Tanzania - Congo - FM Academia - Dunia Kigeugeu

Wednesday, November 24, 2010

Baraza la Mawaziri la Serikali ya Tanzania -2010




OFISI/WIZARA

WAZIRI



1.

Ofisi ya Rais




1.    WN – OR – Utawala Bora
Mathias Chikawe

2.    WN – OR – Mahusiano na Uratibu
Stephen Wassira



2.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma




      Hawa Ghasia


3.

Ofisi ya Makamu wa Rais



1.    Muungano
Samia Suluhu

2.    Mazingira
Dr. Terezya Luoga Hovisa
  


4.

Ofisi ya Waziri Mkuu



1.     Sera, Uratibu na Bunge
William Lukuvi

2.     Uwekezaji na Uwezeshaji
Dr. Mary Nagu



5.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)



George Huruma Mkuchika

Naibu-Aggrey Mwanri

Naibu-Kassim Majaliwa


6.

Wizara ya Fedha



Mustapha Mkulo

Naibu-Gregory Teu

Naibu-Pereira Ame Silima


7.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Shamsi Vuai Nahodha

Naibu-Balozi Khamis Suedi Kagasheki


8.

Wizara ya Katiba na Sheria



Celina Kombani





9.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa




Bernard K. Membe

Naibu-Mahadhi Juma Mahadhi


10.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa



Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi


11.

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi




Dr. Mathayo David Mathayo

Naibu-Benedict Ole Nangoro


12.

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia



Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Naibu-Charles Kitwanga


13.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi



Prof. Anna Tibaijuka

Naibu-Goodluck Ole Madeye


14.

Wizara ya Maliasili na Utalii





Ezekiel Maige


15.

Wizara ya Nishati na Madini





William Mganga Ngeleja

Naibu-Adam Kigoma Malima


16.

Wizara ya Ujenzi





Dr. John Pombe Magufuli

Naibu-Dr.Harrison Mwakyembe


17.

Wizara ya Uchukuzi





Omari Nundu

Naibu-Athumani Mfutakamba


18.

Wizara ya Viwanda na Biashara





Dr. Cyril Chami

Naibu-Lazaro Nyalandu


19.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi




Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu- Philipo Mulugo


20.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii





Dr. Haji Hussein Mpanda

Naibu-Dr Lucy Nkya


21.

Wizara ya Kazi na Ajira





Gaudensia Kabaka

Naibu-Makongoro Mahanga


22.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto




Sophia Simba

Naibu-Umi Ali Mwalimu



23.

Wizara ya Habari, Vijana na Michezo





Emmanuel John Nchimbi

Naibu-Dr Fenella Mukangara




24.

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki



Samuel John Sitta

Naibu-Dr. Abdalah Juma Abdallah








Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika





Prof. Jumanne Maghembe

Naibu-Christopher Chiza




26.

Wizara ya Maji





Prof. Mark James Mwandosya

Naibu-Eng. Gerson Lwinge




Monday, November 15, 2010

Matokeo ya Uchaguzi-TCA

Wajumbe wa mkutano mkuu wa TCA kwa pamoja walichagua viongozi wao wa jumuia kulingana na matakwa ya katiba. Zifuatazo ni picha na majina ya viongozi wapya.

Aliko Mwakatobe-Mwenyekiti

Patrick Kamera-Katibu

Yasmin Kassam-Mweka Hazina

Richard Mwakijale-Mwenyekiti Vijana
Rami Hamisi-Mwenyekiti Uanachama
Adam Kasela-Mwenyekiti Jamii/Starehe
Dr Donatus Mutasingwa-Mwenyekiti Elimu

Wajumbe wa mkutano mkuu na viongozi wapya.