Monday, August 30, 2010

Msiba Ireland na Tanzania

Marehemu Mnomba Njaidi
Kwa niaba ya familia na ukoo wa Njaidi, tunasikitika kutangaza kifo cha ndugu na rafiki yetu, MNOMBA NJAIDI kilichotokea ghafla Ijumaa ya tarehe 27 August 2010 huko Ireland. Marehemu alipendwa sana na wengi lakini Muumba alimpenda zaidi - tunamwombea mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina. Maombi ya Ushirikiano: Kwa niaba ya familia na marafiki wa marehemu, tunaomba msaada wa hali na mali toka kwa watanzania wote waliowahi na ambao hawakuwahi kumfahamu. Michango yenu ya hali na mali inatakiwa ili kufanikisha usafirishaji wa mwili wa ndugu na rafiki yetu kuelekea Tanzania (Toka Ireland). Kwa michango tafadhali tumia details zifuatazo; United Kingdom: Account name: Y W Mirambo Account number: 726 59 181 Sort Code: 09-01-26 Bank: Santander Bank International transfer number: Above details zitafaa lakini namba tutaweka hivi karibuni kurahisisha International transfers Simu: Yusuph +44 7972256826, Munde +44 7869410750, Chambi +44 7900626410 ASANTENI KWA NIABA YA FAMILIA YA MAREHEMU NA MUNGU AWAJAALIE NA AWAONGEZEE SABA MARA SABINI Mungu alitoa na Mungu ametwaa
Jina lake litukuzwe
- Amen!!

Monday, August 23, 2010

Sherehe ya kuzaliwa mzee Omari.

Mzee Omari akikata keki na wajukuu zake kutoka katika jumuiya ya watanzania Kwa niaba ya wanajumuiya tunamtakia Mzee Omari afya njema na kila la kheri!

Tuesday, August 17, 2010

Toronto Fc yaifunga Cruz Azul

Timu ya soka ya Toronto ambayo inashiriki katika ligi ya Mls(Major League Soccer) leo imeingia kwa kishindo katika ligi ya mabingwa kwa upande wa America (Concacaf )baada ya kuifunga timu ya Cruz azul ya Mexico. Ushindi umepatikana kwa mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Mista katika kipindi cha kwanza, Cruz Azul walipata bao la kufutia machozi katika kipindi cha pili. Mpachika mabao wa leo-Mista.

Monday, August 16, 2010

Futari ya Pamoja

Kwa niaba ya wanajumuia ningependa kuwashukuru wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuandaa futari kwa wanajumia wenzao wa jiji la Toronto, mwenyezi mungu awaongezee kheri na baraka.
Baadhi ya picha ni kwa hisani ya kiokote.blogspot.com

Tuesday, August 10, 2010

Ramadan 1431 / 2010 Announcement

Ramadan is on Thursday 12 August, 2010

Ramadan 2010 / 1431 is on Thursday 12th August, 2010

There have been no confirmed sightings of the new crescent in the parameters of the Hilal Committee, therefore Sha'ban will complete 30 days and Ramadan will start Thursday 12th August, 2010.

RAMADAN KAREEM TO ONE AND ALL.

First day of Fasting is on Thursday 12 August, 2010