Sunday, May 30, 2010

Usiku wa kubanjuka-Toronto

The official Bantu Party is here....The hottest party in town . Usiku wa kubanjuka, njooni tufurahi,tucheze, tunywe na tule vyakula vya kinyumbani ......Mandazi, Pilau,Kachori, Katless,Sambusa, Chapati,Vitumbua ,Bajia,nyama choma, na vingine viiiiiiiiiiingi |ALL FREEEE!!!!!! !!!!| doors open @9pm. You don’t want to miss this event... music by the hottest DJ in town….. Usingoje kusimuliwa!! .Come and party untill morning.
Date: Saturday ,July 10th/2010
Location:
101 Lotherton Pathway, North York, Ontario. M6B 2G6
Contacts
Aisha| 647-520-9842
Dora| 647-204-5509

Wednesday, May 26, 2010

50 Cent achonga

Mwanamuziki maarufu wa hiphop nchini marekani amepungua uzito kiasi cha kushangaza watu, Fiddy kama baadhi wanavyomuita amepungua toka 216 mpaka 140 kwa kunywa vimiminika na mazoezi mengine. Yote haya ni katika kutengeneza filamu ambayo amecheza kama mchezaji wa Football aliyeugua kansa, sinema hiyo itaitwa Things Fall Apart, kwa wapenzi wake wasiwe na wasi kwani ameshaanza kula baada ya kumaliza kazi na atarudia afya na mwili wake wa kawaida.

Sunday, May 23, 2010

Harusi Ya Moshi na Nicole

Bwana na Bibi harusi hapo juu, picha za chini ni wanajumuiya waliohudhuria. Bwana Moshi Sakala na Bi Nicole Trotman wakigonganisha glass baada ya kufunga pingu za maisha jijini Toronto hapo jana tarehe 23 Mei 2010.

Saturday, May 8, 2010

Toronto Fc yazima Chicago Fire

Toronto Fc imeichapa timu ya Chicago Fire kwa mabao 4-1, mchezo huo ulikuwa leo katika kiwanja cha BMO field jijini Toronto.Kwa ushindi huu Toronto bado inashikilia rekodi yake ya kutofungwa kwenye uwanja wa nyumbani tokea msimu huu uanze. Chad Barrett aliongoza katika magoli baada ya kupachika magoli 2 dhidi ya timu yake ya zamani, magoli mengine yalipachikwa na O'brien white pamoja na Nick labrocca. Toronto watacheza na Monteal Impact tarehe 12 May. Picha na TFC website.

Man U na Celtic kucheza Toronto July 16

MIGHTY Man U aka THE RELIGION CELTIC FC Timu za Manchester United ya Uingereza na Celtic ya Scotland, zinatarajia kupambana Jijini Toronto katika mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika tarehe 16 Julai mwaka huu. Mpambano huo wa kirafiki utafanyika katika uwanja wa Rogers centre zamani ikiitwa Sky Dome, pambano hilo linatarajiwa kuanza saa mbili za jioni siku hiyo ya ijumaa. Tiketi zitapatikana kupitia mtandao au wakala wa Ticketmaster popote walipo. Viingilio katika mpambano huo vitakuwa ni dola 75 mpaka 150 na tiketi zitauzwa siku ya tarehe ishirini mwezi Mei, kwa wale wapenzi wa mpira kazi kwenu. Esmail.

Monday, May 3, 2010

ELIZABETH BADO HAJAPATIKANA

Elizabeth Chirwa pichani juu, bado hajapatikana ingawa kumekuwa na habari za kuonekana kwake katika maeneo kadhaa ya mjini.kwa yeyote atakayemuona tafadhali toa taarifa katika kituo cha polisi. Mara ya mwisho Elizabeth ameonekana katika maeneo ya karibu na Eaton Center, polisi bado wanaendelea na msako katika maeneo aliyeonekana Elizabeth mara ya mwisho