Sunday, November 28, 2010

REAL MADRID FC KUPAMBANA NA BARCELONA FC -KESHO

Lile pambano linalosubiriwa kwa hamu la miamba ya soka nchini Hispania,Real Madrid na Barcelona, limewadia. Zikiwa zimebakia saa chache wachezaji wa pande zote mbili wanaashiria kutoogopa timu pinzani au mpambano huo kwa ujumla.
Real Madrid chini ya kocha Jose Mourinho, inaingia kwenye pambano hilo ikiwa haijapoteza mchezo kwa kushinda mechi kumi na sare mbili.Kwa upande wa Barcelona wao wana rekodi ya kushinda mechi kumi sare moja na kupoteza mchezo mmoja.
Kukiwa hakuna majeruhi kwa pande zote mbili, mpambano huo unatarajiwa kuwa mkali kwani kumbukumbu zinaonyesha, toka walipokutana kwa mara ya kwanza mwaka 1902, Madrid imeshinda mara 85 na Barcelona 81 huku kukiwa na sare 42.
Mchezaji nyota wa Real Madrid, Christiano Ronaldo amesema wao wanakwenda Camp Nou kwa nia ya kutafuta ushindi na si vinginevyo wakati Lionel Messi,mshambuliaji hatari wa Barcelona, raia wa Argentina, alikaririwa akisema hivi karibuni kwamba Barcelona bado ni timu bora kuliko wapinzani wao, ingawa anakubali kuwa bidii na moto wa Madrid mwaka huu ni tofauti na misimu miwili iliyopita.
Mourinho anatarajia kupunguza “uteja” wa Madrid kwa Barcelona chini ya Guardiola, wakati Mourinho akitamba kuujua mpambano huo hata akiwa usingizini.Madrid hawajaifunga Barcelona nyumbani toka desemba ya 2007 na Mourinho ameshaifunga Barcelona akiwa kocha wa Chelsea na Inter Milan.Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kocha Jose Mourinho kuiongoza Real Madrid katika mpambano na Barcelona.
Ushindi katika El Classico unachukuliwa kuwa ni ishara ya ushindi wa ligi kwani katika misimu sita iliyopita, mshindi wa mpambano huu ndiye aliyechukua kombe mwisho wa msimu.Jumla ya mashabiki 98,000 wanatarajiwa kushuhudia mpambano huo ndani ya Uwanja wa nyumbani wa Barcelona,Nou Camp,huku mamilioni ya mashabiki wa soka ulimwenguni wanatarajiwa kuufuatilia mpambano huo kupitia luninga na mtandaoni.

Nyota wa pande zote mbili wamekuwa na ari ya kutaka kuonyesha vipaji na uwezo wao wakati Ronaldo na Messi wakimimina mvua za magoli katika mechi za karibuni.Huu unaaminika kuwa pia mpambano baina ya Ronaldo na Messi katika kuonyesha nani ni bora zaidi miongoni mwao.
Zote hizi ni dondoo tu, mpira huchezwa kwa dakika tisini.Tusubiri matokeo.
Written by E.Manambi with additional notes by Jeff Msangi


Tanzania - Congo - FM Academia - Dunia Kigeugeu

Wednesday, November 24, 2010

Baraza la Mawaziri la Serikali ya Tanzania -2010




OFISI/WIZARA

WAZIRI



1.

Ofisi ya Rais




1.    WN – OR – Utawala Bora
Mathias Chikawe

2.    WN – OR – Mahusiano na Uratibu
Stephen Wassira



2.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma




      Hawa Ghasia


3.

Ofisi ya Makamu wa Rais



1.    Muungano
Samia Suluhu

2.    Mazingira
Dr. Terezya Luoga Hovisa
  


4.

Ofisi ya Waziri Mkuu



1.     Sera, Uratibu na Bunge
William Lukuvi

2.     Uwekezaji na Uwezeshaji
Dr. Mary Nagu



5.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)



George Huruma Mkuchika

Naibu-Aggrey Mwanri

Naibu-Kassim Majaliwa


6.

Wizara ya Fedha



Mustapha Mkulo

Naibu-Gregory Teu

Naibu-Pereira Ame Silima


7.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Shamsi Vuai Nahodha

Naibu-Balozi Khamis Suedi Kagasheki


8.

Wizara ya Katiba na Sheria



Celina Kombani





9.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa




Bernard K. Membe

Naibu-Mahadhi Juma Mahadhi


10.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa



Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi


11.

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi




Dr. Mathayo David Mathayo

Naibu-Benedict Ole Nangoro


12.

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia



Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Naibu-Charles Kitwanga


13.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi



Prof. Anna Tibaijuka

Naibu-Goodluck Ole Madeye


14.

Wizara ya Maliasili na Utalii





Ezekiel Maige


15.

Wizara ya Nishati na Madini





William Mganga Ngeleja

Naibu-Adam Kigoma Malima


16.

Wizara ya Ujenzi





Dr. John Pombe Magufuli

Naibu-Dr.Harrison Mwakyembe


17.

Wizara ya Uchukuzi





Omari Nundu

Naibu-Athumani Mfutakamba


18.

Wizara ya Viwanda na Biashara





Dr. Cyril Chami

Naibu-Lazaro Nyalandu


19.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi




Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu- Philipo Mulugo


20.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii





Dr. Haji Hussein Mpanda

Naibu-Dr Lucy Nkya


21.

Wizara ya Kazi na Ajira





Gaudensia Kabaka

Naibu-Makongoro Mahanga


22.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto




Sophia Simba

Naibu-Umi Ali Mwalimu



23.

Wizara ya Habari, Vijana na Michezo





Emmanuel John Nchimbi

Naibu-Dr Fenella Mukangara




24.

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki



Samuel John Sitta

Naibu-Dr. Abdalah Juma Abdallah








Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika





Prof. Jumanne Maghembe

Naibu-Christopher Chiza




26.

Wizara ya Maji





Prof. Mark James Mwandosya

Naibu-Eng. Gerson Lwinge




Monday, November 15, 2010

Matokeo ya Uchaguzi-TCA

Wajumbe wa mkutano mkuu wa TCA kwa pamoja walichagua viongozi wao wa jumuia kulingana na matakwa ya katiba. Zifuatazo ni picha na majina ya viongozi wapya.

Aliko Mwakatobe-Mwenyekiti

Patrick Kamera-Katibu

Yasmin Kassam-Mweka Hazina

Richard Mwakijale-Mwenyekiti Vijana
Rami Hamisi-Mwenyekiti Uanachama
Adam Kasela-Mwenyekiti Jamii/Starehe
Dr Donatus Mutasingwa-Mwenyekiti Elimu

Wajumbe wa mkutano mkuu na viongozi wapya.

Sunday, October 10, 2010

ARI MPYA

Wanachama wa TCA pamoja na Viongozi wanaomaliza muda wao kwa pamoja, wamemchagua ndugu Patrick Kamera kuwa msimamizi wa uchaguzi mkuu ujao.

Ndugu Kamera ni mwanachama wa siku nyingi TCA na kazi yake kubwa itakuwa ni kuandaa tarehe ya uchaguzi, mahala pa kufanyia uchaguzi ikiwa pamoja na jinsi ya kufanya uchaguzi.

Katika mkutano huo mambo mengi yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na marekebisho ya katiba ambayo inatakiwa iendane na mahitaji ya wanachama katika muda huu,vilevile wanachama walipendekeza mawazo mbali mbali ambayo yatapelekea chama kuwa na muelekeo mpya,ikiwa ni pamoja kuendeleza yote mazuri ambayo yamefanywa na uongozi unaomaliza muda wake.

Mkutano huo ulichukua pia nafasi ya kupendekeza majina ya baadhi ya wanachama ambao inadhani wana nia na uwezo wa kushika nafasi mbali mbali za uongozi, tarehe na taratibu zitakazofuata zitatangazwa hapo baadaye.

Kwa ufahamu tu TCA ilianzishwa mwaka 1990 na watanzania wachache ambao waliona umuhimu wa kuwa na jumuia ambayo itawaweka pamoja wahamiaji toka Jamhuri ya muungano wa Tanzania, mpaka muda huu TCA ina miaka Ishirini.

Walioketi ni viongozi wanaomaliza muda wao na nyuma yao ni viongozi wanaotarajiwa kuingia madarakani, mwenye mvi ni mmoja wa waanzilishi na mstaafu Mzee Omari Mwinyi.

Monday, October 4, 2010

MKUTANO-TCA

Ndugu Wanachama wa TCA, Naomba kuwakumbusha kuwa tutakuwa Mkutano Mkuu wa Mwaka Jumamosi Tarehe 9 Oktoba kwenye ukumbi uliopo 105 Weldrick Road East, Richmond Hill, ON L4C 9Y9, kuanzia saa tisa mchana hadi saa kumi na mbili (3:00PM to 6:00PM). Huu ni mkutano wa wanachama tu lakini wale wasio wanachama wanakaribishwa kuhudhuria na kujiandikisha uanachama kabla mkutano haujaanza.Vilevile wanachama wote wanatarajiwa kulipia ada ya mwaka ya uanachama siku hiyo ya mkutano. Wote mnakaribishwa, Ahsanteni, Bashir Kassam MWENYEKITI, TCA

Monday, September 27, 2010

Friday, September 17, 2010

Tangazo toka TCA

Hello Wanachama, Kwa niaba wa bodi ya TCA napenda kuwafahamisha kuwa tarehe rasmi ya Mkutano Mkuu wa chama pamoja na uchaguzi wa viongozi wapya utafanyika tarehe Jumamosi 9 Oktoba 2010 kuanzia saa 9 mchana hadi saa 12 jioni. Taarifa zaidi zitafuata. Rgds Prosper Katibu Mtendaji, TCA

Monday, September 13, 2010

Sunday, September 12, 2010

A SPECIAL MESSAGE FROM UMOJA BASH ORGANIZERS

Jeff, Dj Dennis and Esmail.

Dear friend,

From the deep of our hearts, we want to THANK YOU for coming to the 1st Annual Umoja Bash, 2010 last night. We enjoyed every aspect of having you there and we hope you enjoyed it too and above all, you had a great time.

So far, we have received wonderful and supportive feedback from many of you. It was indeed one of the most terrific nights and quite memorable. That was all made possible because of people like you who came out in such a historic number despite the rainy weather.

It was great to have so many from East Africans under one roof without forgetting our friends and supporters from all other parts of the world. We are so grateful to all of you who made extra efforts to make sure that everyone who wanted to attend got an opportunity to do so.

Special Thanks to our sponsors DukaTech and our super charged and supportive volunteers. Thanks to our amazing DJ Dennis (Skinny D) who flew all the way from Minneapolis, Minnesota to be part of this great event.

Lastly, since this was our first event, we would like to get your feedback as we move forward in creating even better events in the near future and especially the 2nd Annual Umoja Bash next year. You can e-mail us with your feedback at esmaez@yahoo.ca or jeffmsangi@gmail.com or sollohokal@yahoo.com .

THANK YOU, THANK YOU, THANK YOU

Esmail, Jeff and Solo

Thursday, September 9, 2010

EID Mubarak!

Eid Al Fitr will be on Fri 10 September, 2010

EID Mubarak!


Based on verified reports of crescent sightings in Trinindad and Guyana on the eve of Thursday September 9th 2010 (29 Ramadan), the Hilal Committee of Toronto has declared the 1st of Shawwal 1431 to be on Friday 10 September 2010. Eid ul Fitr will be on Friday 10 September 2010 The Hilal Committee with it's membership of more than 80 organizations wishes one and all a blessed and joyful Eid ul Fitr.

Sunday, September 5, 2010

Maombi Nyumbani kwa Bashir na Sandra

Watanzania tulikusanyika hapo jana nyumbani kwa Bashir na Sandra kwa ajili ya maombi ya marehemu Charity ambaye ni dada ya Sandra,msiba umetokea huko nchini Afrika ya kusini na Sandra anatarajia kuondoka leo kuelekea kwenye shughuli za mazishi.